GET /api/v0.1/hansard/entries/615544/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 615544,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615544/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingara na Rasilimali kwa kuleta Hoja hii. Ikiwa Serikali itafuata Hoja hii inavyotakikana, itakuwa ya maana sana. Watu wa Pwani, kwa mfano Mombasa na Kwale, wamekuwa wakisumbuka na kuteseka sana kwa sababu ya hali ya kutoweza kumudu shughuli zao. Serikali ilikuwa inawaachilia watu kuingililia Mwambao wa Pwani bure tu na kuvuruga mambo. Nina imani kwamba, kutokana na Hoja hii, mambo yatakuwa sawasawa. Naiomba Serikali ifuatilie mambo haya baada ya hapa. Kama vile Mheshimiwa alivyozungumza, miradi mingine kama ule wa kuchimba makaa ya mawe kule Lamu ni miradi ambayo ni haki kabisa izuiliwe mapema. Tatizo ni kwamba shughuli za Katiba ziko wazi, watu wanapitisha sheria, lakini mambo yanafanywa kimabavu na kunatokea mambo ambayo hayastahili. Kwa mfano, kule Mwambao wa Pwani katika Kaunti ya Kwale kuna uvuvi ambao unapaswa ufanyike vizuri. Lakini utaona kwamba kwa sababu hakuna ushirikiano, uelewano na umoja kati ya Serikali ya kitaifa, serikali ya kaunti na wananchi, miradi inayofanywa pale si miradi mizuri, na inafanywa kwa kutumia nguvu. Juzi, halmashauri ya Bandari ya Mombasa, walichimba mchanga kule na kuvuruga kila kitu kwa sababu hakuna usimamizi bora. Ikawa wananchi wanakosa kufanya shughuli zao za uvuvi kwa muda mrefu na samaki wakapotea kwa sababu ya uchimbaji wa mchanga ambao haukuwa sawa. Naunga mkono kikamilifu Hoja hii. Lakini, naomba Serikali ifuatilie na ifanye vile ambavyo Bunge hili la Kenya, ambalo ni tukufu na linakubalika, litakuwa limepitisha."
}