GET /api/v0.1/hansard/entries/615549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 615549,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615549/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "mabadiliko. Hawakuhusishwa katika mabadiliko hayo, wala hawajui kitu gani kinaendelea. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu maisha ya watu wa Pwani yataendelezwa kwa kufanya miradi tofauti tofauti ya kuleta maendeleo katika sehemu hiyo. Ni aibu kuwa nchi ya Kenya inashindwa na nchi ndogo kama vile Mauritius, ambayo imeendelea sana katika maswala ya uvuvi, ilhali ni nchi ndogo sana na yenye watu wachache sana; ni lazima tujiendeleze. Pia, nimegundua kuwa mara nyingi Serikali haiwaajiri watu wa Pwani wala haihusishi watu wa Pwani katika miradi ya Pwani. Nilienda mkutano kule Mauritius, na kati ya Wakenya 11 tuliosafiri, mimi pekee ndiye nilikuwa nimetoka Pwani. Sikutoka katika Wizara. Ulikuwa ni mkutano wa Wizara. Yaonekana kuwa kwa sababu watu wa Pwani hawahusishwi sana katika maswala, ndio sababu tangu tupate Uhuru, maswala ya uvuvi yamekuwa nyuma sana. Hii ndio maana tunapitwa na nchi nyingine kama Norway, nchi ndogo sana, lakini katika ulimwengu mzima ndio ya pili katika kuuza samaki. Ya kwanza ni nchi ya Uchina. Hapa Kenya, tunaweza kupunguza umaskini ikiwa tutazingatia mambo yaliyotajwa katika hii Ripoti. Isiwe tu ni ripoti ambayo itakaa na kupata vumbi, lakini iwe Ripoti ambayo mambo yake yatafuatiliwa. Jambo lingine ni kwamba katika bajeti za masuala ya uvuvi na kadhalika, pesa nyingi sana huwa zinaenda kwa utafiti. Mwaka baada ya mwaka, Bajeti ikitengenezwa, hata tukijaribu kushindana, pesa nyingi sana zinaelekezwa kwenye utafiti. Saa hii tunataka pesa zielekezwe katika masuala ya maendeleo, kwa sababu baada ya miaka hiyo yote hatujaona faida ya huo utafiti. Kitu kingine ni, kama alivyozungumza Mhe. Mwanyoha, uchimbaji wa mchanga umefukuza samaki, na wavuvi hawana njia nyingine ya kupata pesa. Umaskini umezidi sasa. Mashirika ya kusimamia ufuo wa bahari pia yameachwa peke yao. Hawashugulikiwi na Serikali. Pesa haziko ilhali wanafanya kazi nzuri. Kumalizia, nashukuru sana Mwenyekiti na wanachama wa Kamati hii kwa kuleta Hoja hii."
}