GET /api/v0.1/hansard/entries/615771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 615771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615771/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe maoni yangu kuhusu uteuzi wa Daktari Muraguri. Dunia hii ni duara na rangi rangile. Naomba nikimuunga mkono huyo daktari, wakumbuke waliyonitendea wakati tulipewa fedha – Shilingi milioni mia moja katika hospitali ya Wesu Taita. Mhe. Spika, wamenizungusha huku na kule wakiniambia nilete orodha ya vifaa na mashine ambazo nahitaji. Niliwakabidhi lakini mpaka leo, Dr. Muraguri na wenzake wameshindwa kueleza vile walivyotumia fedha hizo na vifaa walivipeleka wapi. Hayo yalifanyika katika Bunge la Kumi. Ni ombi langu kwa sababu amepewa nafasi ya kuchukua wadhifa wa kuendesha Wizara ya Afya. Kwa yale madhambi aliyonifanyia, nimemsamehe. Nafikiri ataanza upya kufanya kazi ninavyomtarajia. Daktari Muraguri amekuja wakati ugatuzi umeingia. Nina imani ataweza kufanya kazi sawasawa. Nina imani ataweza kuangalia madaktari wale ambao wana sifa na ambao wanahitajika kufanya kazi katika sehemu zote za nchi. Wakati huu Daktari Muraguri anachukua nafasi hii, ni wazi kuwa kuna matatizo chungu nzima katika Wizara ya Afya. Ni matumaini na matarajio yangu kuwa Daktari Muraguri, akishirikiana na Daktari Cleopa, watafanya kazi ambayo inahitajika na kuwa hawatawaaibisha watu ambao wamewapatia kazi hii. Kila wakati, tunakemea Serikali kuhusu ufisadi. Ukiangalia mara nyingi, wagonjwa wameenda mahospitali makubwa wakaambiwa: “Msipotoa mlungula, hampati chochote. Usipotoa hiki, hutibiwi.” Nina imani Daktari Muraguri atachukua nafasi hii kuhakikisha kwamba yale yote yaliyokuwa yakitendeka katika Wizara yamerekebishwa. Naunga mkono."
}