GET /api/v0.1/hansard/entries/615818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 615818,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615818/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "ndoto kubwa, matarajio makubwa na mipango mikubwa ya kusema kwamba wataweza kuangamiza hili jinamizi la ufisadi hapa nchini Kenya. Lakini tumeendelea tukiona kwamba ufisadi umeendelea kuzorotesha nchi yetu pamoja na uchumi wetu. Kwa hivyo, wajue kwamba Wakenya wote wanawaangalia ili tujue ni watu wangapi watapelekwa jela . Kusema kwamba mtu yeyote ambaye ametajwa katika mambo ya ufisadi akae kando ama atoke kazini tu, hiyo haisaidii.Wakati wanakaa kando ama wakati wanaacha kazi ni vizuri tupate kujua kama Wakenya hizo fedha wameiba, kama kunao ushahidi wowote kwamba wameiba hizo fedha, zitapatikana vipi na zitarudishwa vipi. Singeweza kutaja wote ambao wamewekwa hapo mbele lakini nitagusia kuhusu dada yetu Rose Mghoi kwa sababu mara ya kwanza aliletwa katika Bunge hili, hakuweza kupata nafasi hiyoi. Ni maombi yangu kwamba wakati huu ataweza maanake kulingana na zile kazi ambazo amefanya hapo mbeleni, inaonekana kwamba amehitimu kufanya kazi ya kupambana na ufisadi. Vile vile, ameketi katika Tume ya Utekelezaji wa Katiba, kumaanisha anakielewa Kipengele cha Sita kinachohusiana na mambo ya maadili---"
}