GET /api/v0.1/hansard/entries/615831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 615831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615831/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Ni Tume ya kupambana na ufisadi. Tunashukuru sana Rais wetu kwa kuangalia pembe zote za Kenya kwa sababu kuna Wakenya wengi ambao hawajawahi kuingia kwa hizi bodi na ndani ya mambo ya Serikali. Saa hii, tunaona kwamba Wakenya wote wameangaliwa pembe zote. Kwa kusema ukweli, ufisadi katika Kenya ni kali sana na ni mbaya. Sisi wote tunapambana na ufisaidi. Nataka kusema ya kwamba hawa wenzetu ambao wamechaguliwa kuwa kwa hiyo ofisi ni muhimu pia tuwapatie nguvu wapate kuangalia pembe zote za Kenya. Hiyo ni kwa sababu kila wakati, inasemekana kuna ufisadi. Sijui kama huu ufisadi unahusika na pesa au ni ya wizi wa ng’ombe. Hii ni kwa sababu kila pahali, unakuta ng’ombe wanaibiwa asubuhi na jioni na haifuatiliwi. Sasa sijui kama hiyo ni ufisadi au wizi. Kwa hivyo, ningeomba wenzangu wale wamechaguliwa kuhudumu katika hiyo ofisi waangalie wizi wa ng’ombe. Kwanza, tuzungumzie jambo hilo kwa sababu watu wamekuwa maskini."
}