GET /api/v0.1/hansard/entries/615959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 615959,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615959/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ninampongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuona kwamba hawa ndugu zetu wawili, Charles Sunkuli na Dkt. Margaret Mwakima, wanafaa kuhudumu katika Serikali yake. Kamati yetu pia imewapiga msasa na tukaona kwamba wanafaa. Mimi ninaomba niunge mkono uamuzi na uteuzi huu ili hawa ndugu zetu wawili waingie kwenye Serikali. Bila shaka, wataboresha shuguli za Serikali na kujaza pengo pale ambapo kumeonekana kuna upungufu. Hawa wote wanatoko kwenye sehemu ambazo zinaangalia mazingara na mali ya asili. Bw. Sunkuli, akiwa anatoka sehemu za Narok; na Bi. Mwakima, akiwa anatoka sehemu yangu ya Taita, ambayo ninawakilisha. Kwangu ni fahari kuona tunaweza kutoa mmoja wetu akaweza kupata nafasi ya kuhudumu katika Serikali. Nina imani, wasipoingia serikalini na kuanza uchafu, wao ni watu ambao wanasifa na uzoefu. Bila shaka, wataweza kumudu nafasi ambazo wamepewa. Ninaimani kwamba hawataenda huko na kushika tabia mbaya ambazo tumeziona katika serikali fisadi, bali watakuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba wameboresha utendakazi katika sekta ambazo wamepewa wasimamie. Ninayaunga mkono yale yote ambayo yamesemwa na Mwenyekiti – kwamba wafanyikazi wa Umma wapatiwe sera na wasomeshwe kidogo angalau wapate uadilifu utakaowawezesha kuhudumia Serikali ipasavyo. Haswa, inafaa wapewe mafunzo mwafaka kuhusu matumizi ya fedha za umma, yakiwemo mafunzo mengine mengi yanayohitajika kuendeleza Serikali. Kwa sababu ya muda, ninaomba tu nitoe shukrani kwa niaba ya watu wa maeneo Bunge ya Wundanyi, Taita Taveta na Narok. Ninatoa shukrani kuwa watu wetu wamepatiwa nafasi ijapokuwa ni wachache. Wengine wako. Mkiwahitaji pia tunaweza kuwapatia. Ahsanteni na ninawatakia kila la heri."
}