GET /api/v0.1/hansard/entries/616080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616080/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Nakushukuru sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono uteuzi wa maafisa ambao wamepata nafasi ya kufanya kazi ya muhimu sana katika Kenya hii. Sisi sote twajua kwamba twategemea sekta ya kilimo. Kama tutaweza kupata watu wazuri kusimamia ukulima, sisi sote tutafaidika katika Kenya kwa sababu hatujafika kiwango cha kupata chakula cha kutosha. Litakuwa jambo muhimu sana tukiwa na maafisa ambao wataweza kutuongoza kwa njia nzuri ili tuweze kupata chakula cha kutosha. Mimi naunga mkono Hoja hii kwa sababu hiyo. Nashangaa kuwaona Wabunge wengine wakisimama hapa kana kwamba siyo Wakenya. Wanasimama hapa wakitaka kuendeleza ukabila. Wengine wanataka kufanya siasa waonekane wanatetea makabila yao ili wapate kura. Hilo si jawabu. Jawabu letu ni tuwaunge Wakenya mkono. Mtu yeyote anaweza kuisaidia Kenya hii bila kujali ametoka eneo lipi la Kenya. Mtu akichaguliwa huwa ni asaidie nchi. Tunajua kuna wale huwaza kwamba pengine hawawezi kuchaguliwa tena 2017 na kwa hivyo, lazima watafute njia ya ukabila ili wakitoka waseme walitetea makabila yao. Hao ni watu wameanguka na ambao hawana sura ya Kenya. Kuna watu ambao wanakaa wakingojea. Ningependa watu waende kwa kitabu cha Mungu. Kuna mtu alikaa kwenye kisima kwa muda wa miaka 38 lakini hakuwa na pesa wala nguvu za kuingia kisimani kutibiwa. Kwa sababu ya imani, Yesu alimuona na akamwambia:- “Simama na utembee kwa sababu ya imani yako.” Wale hatujapata, siku moja itafika tutapata kiti. Sisi watu wa Nakuru tuna imani kama ya huyo mtu aliyekaa miaka 38. Hata kama hatujapata tangu 1963, tuna imani kwamba siku moja tutapata na tutaongoza Kenya hii kwa sababu ya imani. Mungu awabariki."
}