GET /api/v0.1/hansard/entries/616191/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616191,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616191/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Aburi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": "Katika Bunge hili, mtu anapokosoa Serikali inasemekana kuwa anapinga Serikali. Sijapinga Serikali lakini watu wote lazima wachukuliwe sawa. Wanatigania tuko wengi. Wakati wa kupiga kura, Mlima Kenya huwa na nyasi na mtu wa Mlima Kenya huambia Wanatigania anawapenda wampe kura. Lakini ikifika wakati wa kula na kugawa, Mlima Kenya humea nyasi na Mtigania haonekani tena. Wakati umefika bendera ya Mtigania ipande juu ili aweze kuonekana nchini Kenya."
}