GET /api/v0.1/hansard/entries/616439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616439,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616439/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nijiunge na wenzangu, nikiwa mmoja wa Wanachama wa Kamati ambayo iliwahoji na kuwakagua wateule wanaopewa nafasi ya kujiunga na Baraza la Mawaziri nchini Kenya. Mhe. Spika, ukweli ni kwamba Mhe. Rais Uhuru Kenyatta ameona umuhimu wa kuwapa Wakenya wengine nafasi ya kuwahudumia Wakenya katika Baraza lake la Mawaziri. Mhe. Kiunjuri alifanya kazi hapa Bungeni kwa mihula mitatu akiwa Mbunge na Naibu wa Waziri. Vile Vile, katika kisomo chake, ana shahada kadhaa. Kazi ambayo anapewa ya kusimamia masuala ya ugatuzi na mipangilio ya nchi hii, ataifanya bila wasiwasi. Mhe. Spika, kama vile wenzangu walivyotaja, jambo la kusikitisha ni kwamba Wakenya wengi wananyimwa haki kwa sababu ya kesi ambazo zimewakabili kwa muda mrefu. Kuna mtu ambaye amejaribu kutumia njia hiyo kuweka fitina ili Mhe. Kiunjuri asipewe nafasi ya kuwahudumia Wakenya kwenye Baraza la Mawaziri. Si sawa Wakenya kunyimwa haki kwa misingi ya watu fulani wanaotumia masuala fulani kuwagonga watu wengine kisiasa. Nikizungumzia suala la Charles Keter, amesomea shahada tofauti. Amewahi kuchaguliwa mara tatu na watu wa Belgut na baadaye kuchaguliwa kama Seneta wa eneo la Kericho. Hii inaonesha watu wa kule kwake wana imani na yeye na anaweza kufanya kazi. Vile vile, alipokuja Bungeni, amefanywa Naibu wa Walio Wengi kwenye Seneti. Ukiangalia ile kazi aliyoifanya kwa Wizara akiwa Naibu wa Waziri, itamsaidia kwa kazi hii anaenda kufanya."
}