GET /api/v0.1/hansard/entries/616441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616441/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Namtakia ndugu yangu Dan Kazungu kila la heri anakokwenda kuwafanyia Wakenya kwa ujumla kazi akituachia shughuli za kisiasa. Wakati tukifanya shughuli hizi, tumeona maswala ya fitina, unafiki na kuzushiwa ili asiweze kupata kazi hii. Bila shaka, tulipoangalia masuala yale, tuliona ya kuwa Dan Kazungu ni kijana ambaye alichaguliwa na wapendwa wake wa Malindi na wamemfurahia. Wametupigia simu wakitoka Kaunti ya Kilifi haswa eneo Bunge la Malindi wakisema kuwa wamefurahia sana kuchaguliwa kwake katika Baraza la Mawaziri. Sina wasiwasi kuwa katika Wizara hii aliyopatiwa ya kusimamia masuala ya madini, ataweza kufanya kazi. Ana shahada mbalimbali za kumwezesha kufanya kazi hiyo. Kuna suala la jinsia ambalo limekuwa likisumbua kila mtu. Nilipochaguliwa kwenye Bunge la Kumi, niliwahi kuwa Waziri kwenya Wizara ya Jinsia. Hivyo basi, nataka kumpongeza Mhe. Rais kuona kuna umuhimu wa kuwa na Wizara ya kusimamia masuala ya jinsia, vijana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}