GET /api/v0.1/hansard/entries/616473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616473,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616473/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Katana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika. Nachukua nafasi hii kuunga mkono mjadala huu ambao tunaujadili sasa kuhusu uteuzi wa mawaziri. Kwanza, namshukuru sana Rais wa Jamuhuri yetu ya Kenya kwa kuwachagua Wakenya ambao Ripoti ya Kamati ya Uteuzi hapa Bungeni inaonyesha kuwa wana tajriba nzuri na elimu ya kutosha ya kuweza kuongoza katika nyadhifa hizo ambazo Raisi amewatunuku. Mimi binafsi, namshukuru sana Rais kwa sababu ya kumteua ndugu yetu Mhe. Dan Kazungu ambaye alikuwa Mbunge wa Malindi. Tunafurahi sana kama watu wa Kilifi na Wakenya na, hususan, wakaazi wa Malindi. Nimemjua Mhe. Dan Kazungu kama kiongozi. Ni mtu ambaye ana tajriba na utaalamu wa kutosha. Hata kama ile Wizara ambayo anaenda hailingani na taaluma aliyo nayo, katika mahojiaho na Kamati ya Uteuzi, Dan Kazungu alifaulu. Nami nampa kongole. Amekuwa Mbunge ambaye amefanya kazi yake kulingana na wajibu wake katika Eneo la Bunge la Malindi. Mimi kama mkazi wa Malindi, nampa kongole sana Mhe. Dan Kazungu. Namtakia kila la heri kwa sababu yale ambayo yalikuwa yanazungumzwa ni maneno ambayo hayajathibitishwa na hayawezi kumzuilia Mhe. Dan Kazungu kushikilia wadhifa huu. Mhe. Dan Kazungu amekuwa kielelezo. Katika uteuzi huu, kuna wakati tulikuwa tunaangalia masuala ya uteuzi wa nyadhifa mbalimbali na tukakosa kuona kwamba Rais ametekeleza masuala ya jinsia. Hapa pia mawaziri wanawake waliotoka ni wawili. Katika kurudisha, alirudisha mwanamke mmoja tu. Namwomba Rais wetu wa Jamuhuri ya Kenya aangalie na asisitize sana masuala ya kina mama katika nyadhifa kuu katika Serikali yake. Mengi yamezungumzwa kuhusu masuala ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC). Naomba sana kwamba yale ambayo yako hivi sasa yaangaliwe kwa kina ili yasihujumu masuala ya wale waheshimiwa ambao wametajwa na uvumi ambao si wa msingi. Kwa hivyo, namuombea kakangu Mhe. Dan Kazungu heri maana ametuongoza Malindi na sasa amepanda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}