GET /api/v0.1/hansard/entries/616562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616562,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616562/?format=api",
    "text_counter": 305,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Kwanza, wakati walikuwa wanapigwa msasa, hawa ndugu zetu Wakenya wameonyosha kisomo ambacho kinafaa, sifa ambazo zinastahili na maadili wanayo ambayo yanahitajika kulingana na Katiba. Kwa hivyo, wamejitoa mhanga watumikie nchi hii. Ni muhimu hawa ndugu zetu watatu ambao wamechaguliwa kuwa Makatibu Wakuu wawajibike. Wasipowajibika watakuwa wanajinufaisha wao wenyewe. Na vile tunavyona nchi inavyoendelea, imekumbwa na mambo mengi ambayo yanahitaji ustadi muhimu sana wa kazi. Inabainika wazi wazi kuwa hawa ndugu zetu watatu wana uzoefu wa kutosha katika nyadhifa mbali mbali ambazo walikuwa wameshikilia kabla ya kuteuliwa kuchukua nafasi hii. Lakini hata hivyo lazima hawa Makatibu waangazie na waangalie wasije wakatumbukia katika lindi la ufisadi. Utakubaliana na mimi kuwa moja ya changamoto ambazo tuko nazo nchini ni ufisadi. Hili ndilo jambo limemfanya Rais akaamua ateue Makatibu Wakuu wapya na aondoe wengine. Kwa hivyo, hawa ndugu zetu ambao wamepatiwa nafasi ya kutumikia nchi hii kama Makatibu Wakuu - Sammy Itemere, Mhandisi Victor Kyalo na ndugu Andrew Kamau Ng’ang’a – ninawasihi na kuwaomba watibitishe kwa wananchi kuwa nafasi hii ambayo wamepatiwa kama Makatibu Wakuu wasije wakaiharibu ila wajibidishe walete nchi karibu. Hasa wasia wangu unaenda kwa Katibu Mkuu ambaye atakuwa anashughulikia mambo ya utangazaji na mawasiliano. Utangazaji na mawasiliano utakuwa unaangazia nchi yote ya Kenya. Kwa hivyo, ni muhimu aboreshe hiyo nafasi na hiyo kazi. Tukiangalia Idara ya Utangazaji ya Kenya, tunapata kwamba imezorota sana. Ni kituo ambacho kimepitwa na wakati na kimeshindwa na wenzake ambao wameingia hivi karibuni. Ninatarajia ndugu Itemere achukue muda wake ahakikishe kwamba ameboresha sera hiyo."
}