GET /api/v0.1/hansard/entries/616576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616576,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616576/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kega",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1813,
        "legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
        "slug": "james-mathenge-kanini-kega"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii ambayo tuko nayo siku ya leo. Kwanza, nitasema kuwa ninashukuru Kamati ya Kawi na Mawasiliano ambayo inaongozwa na Mhe. Jamleck, maanake wamefanya kazi ya ziada. Stakabadhi ambazo wametuletea siku ya leo zimeonyesha taratibu walizozifuata na inaonekana kwamba waliokaguliwa ni watu ambao wanaelewa kazi walizoteuliwa kufanya. Pili, ni vizuri wale ambao wameteuliwa kujua kwamba wameteuliwa kufanyia taifa letu la Kenya kazi. Hawajapatiwa nafasi ya kwenda kule kujitarisha ama kujitafutia umaarufu na mambo kama hayo. Kwa hivyo mimi ninasimama kuunga mkono taarifa ambayo tumepatiwa siku ya leo. Walioteuliwa wana jukumu kubwa mbele yao."
}