GET /api/v0.1/hansard/entries/616587/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616587,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616587/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Abdi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono uteuzi wa maafisa hao waliotajwa katika mjadala huu kuhusu Hoja Maalum ya maafisa walioteuliwa na kuletwa mbele ya Bunge na Rais Uhuru Kenyatta. Tunapowateua watu hawa na kuwapitisha, tusiangalie kwamba wao wanatoka kwetu nyumbani. Tusiangalie kama wao ni wa kabila letu na pia tusiangalie kama wao ni dini yetu bali tuangalie kwamba wao ni Wakenya wanaostahili kuteuliwa katika nyadhifa hizo za kitaifa. Nikizungumzia kuhusu Balozi Peter Kirimi Kaberia, huyu ni mtu ambaye ametumika katika nyadhifa mbalimbali katika taifa letu. Kwanza, alikuwa mwandishi wa habari. Pili, alikuwa afisa katika Wizara ya Ushauri wa Nchi za Nje na Biashara ya Kimataifa na baadaye akawa Balozi nchini Brazil. Katika mahojiano yetu naye katika Kamati ya Ulinzi na Uhusiano na Nchi za Nje, alijitokeza vizuri sana akionyesha uhodari na utendakazi wake. Hasa tulipendezwa sana kwa sababu yeye alikuwa na fikra mpya ambazo sisi kama Wabunge wa Kamati hiyo tunafikiria kwamba zitaendeleza mbele kazi za kila siku za Wizara ya Ulinzi na kuleta nguvu na fikra mpya katika wizara hiyo. Kwa hivyo tunaunga mkono uteuzi wake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}