GET /api/v0.1/hansard/entries/616588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616588,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616588/?format=api",
    "text_counter": 331,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Abdi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Pili, katika uteuzi wa Betty Maina kuwa Katibu katika wizara inayohusika na Shirikisho la Afrika Mashariki, Bi. Maina alionyesha ujuzi wake katika kazi hizo na kuonyesha pia kwamba kwa hakika anastahili kuteuliwa katika kazi hiyo. Ujumbe wangu wa mwisho ni kwamba maafisa hawa wakumbuke kwamba kazi yao ni kujenga Kenya na kuwatumikia wananchi. Lazima wafanye kazi hizo kwa uadilifu na maadili bora na kutia kasi kuendeleza ajenda ya serikali na maendeleo ya nchi hii. Kwa hayo machache Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono uteuzi wa maafisa hawa wazuri wawili ambao walipitia katika Kamati yetu. Asante sana"
}