GET /api/v0.1/hansard/entries/616789/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616789,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616789/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu wa Spika. Kwanza, ingawaje ninaunga mkono Mswada huu, nina dukuduku kadhaa. Hektea 123,000 za ardhi katika sehemu ninayowakilisha Bungeni zimechukuliwa. Shule za msingi na zile za upili, pamoja na hospitali, sasa ziko katika sehemu ya msitu. Nilileta teteze Bungeni mwezi wa nne mwaka uliopita. Kamati husika ya Bunge hili ilitumwa huko na kujionea ukweli wa mambo. Kamati hiyo imeleta pendekezo kwamba mipaka ya misitu katika kaunti ya Tana River, na haswa katika sehemu ya Bura, ibadilishwe. Kwa bahati mbaya ama nzuri, Ibara ya 28 ya Sheria ya Misitu, ambayo ilipitishwa na Bunge kabla ya Ripoti ya Kamati husika kuwakilishwa Bungeni, imeipatia Wizara husika mamlaka ya kubadilisha mipaka ya misitu, licha ya Bunge kupitisha tetezi iliyowakilishwa hapa, baada ya kujionea matatazo yanayowakumba wakazi wa Tana River. Wizara ya Misitu imeshikilia msimamo wake wa awali, na mpaka leo wamekataa kubadilisha mipaka ya misitu katika eneo la Bura. Langu ni kuliomba Bunge hili kwamba, ingawaje sisi wakazi wa Bura tunapenda kuhifadhi misitu, tusichukue ardhi ambako kuna shule za umma, hospitali na vituo vya polisi na kuifanya sehemu ya msitu . Ndiposa ninawaomba Wabunge waniunge mkono ili nilete rekebisho kwa Kipengele cha 33 ili mamlaka ya kubadilisha mipaka ya misitu yaondolewe kutoka kwa Wizara na kuletwa Bungeni ndiyo tukishirikiana na National Land Commission, tuangalie mchakato wa kubadilisha mipaka ya misitu. Kule Tana River, shule ambazo tuko nazo tayari ni chache. Je, Wizara ya Misitu ikizifunga kwa madai ya kuwa ziko katika sehemu za misitu, licha ya kwamba gazetttment The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}