GET /api/v0.1/hansard/entries/616795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616795,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616795/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Wananchi hao wako na shida sana. Hata mimi, na miaka yangu yote, nilizaliwa ndani ya msitu huo. Watu hawana shule, hospitali ama maji, na wanateseka. Mara kwa mara, wanaambiwa wahame kutoka kwa msitu. Kwa hivyo, ni muhimu mipaka ya misitu ijulikane ili wananchi pia wapate kujua iwapo wanaishi msituni ama la. Hii ni kwa sababu tumesumbuka sana katika Kaunti ya Samburu. Katika baadhi ya sehemu hizo, shule zilijengwa miaka 40 iliyopita na watu sasa hivi wanambiwa wahame kwa sababu makazi yao yako katika sehemu ya msitu. Kwa hivyo ni muhimi mipaka katika makazi ya wananchi na misitu ijulikane. Kuna mpaka ambao umechorwa mara mingi. Kila mwaka huo mpaka uko kwa ramani nyingine. Ramani zinatolewa kila wakati. Wananchi wanaishi kwa njia ambayo haistahili na watoto wao hawaendi shule. Nikiwa mwakilishi wa Kaunti ya Samburu, nimesema kuwa hapo wanapoishi watakuwa na shule. Tumeagana na gavana wetu tukasema lazima tuweke shule na hospitali ili watu wapate njia ya kujisaidia. Mara kwa mara wanaambiwa wako kwa msitu na hawako msituni. Kwa hivyo ni vizuri mpaka ujulikane. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}