GET /api/v0.1/hansard/entries/616807/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616807,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616807/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante Mheshimiwa Naibu wa Spika. Ninaomba nami nitoe mchango wangu kwa Mswada huu ambao uko Bungeni leo. Tukubaliane kwamba misitu ni moja ya raslimali za nchi hii, ambazo zinahitaji kulindwa na kuhifadhiwa. Mutakubaliana nami kwamba nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa ya kuridhisha katika jitihada za kuhifadhi misitu. Ijapokuwa Mswada huu unaangazia changamoto ambazo zitakuwepo, ni muhimu tuangazie matatizo ambayo yapo katika uhifadhi wa misitu yetu nchini Kenya. Wakenya kwa ujumla ni watu ambao wanapenda miti na wanapenda kuhifadhi mazingira lakini mara nyingi wanavunjwa moyo na wale ambao wamepatiwa majukumu ya kuangalia na kutunza misitu yetu. Naomba kwa ufupi tu niangazie sehemu ya Taita Taveta ambayo ina misitu inayojulikana ulimwenguni kama misitu ya Mwandango, Ngangao, Vuria na Susu. Misitu hii ina miti ya kienyeji ambayo imekuwa kwa muda wa miaka mingi. Shida ni kwamba unakuta wale wanaopatiwa nafasi ya kuvuna hii misitu wanakuja na hawaangalii nani wamehifadhi hii misitu. Wananchi wamehifadhi hii misitu na wameingalia na kuhakikisha kuwa haiharibiki. Watu wanapewa kibali na kukata miti kiholela. Wale wananchi ambao wameshughulika kuhifadhi hii misitu hawana chochote cha kusema. Hao maofisa ambao wamepatiwa majukumu ya kuangalia na kutunza misitu yetu wamekuwa chanzo cha kwanza kuharibu hiyo misitu. Ukienda pale Wundanyi, vibali vinatolewa kiholela. Hata juzi, imebidi watu washikwe. Walienda msitu wa Mwandango kuvuna miti tunayoita Sandalwood ambayo inahitajika kuhifadhiwa na kutunzwa. Naomba niwapongeze Naibu Kamishna wa Kaunti kwa kuhakikisha kuwa watu hao wameshikwa. Ijapokuwa walitoroka, gari lao limeshikwa ambalo nia yake ni kuangamiza msitu ya Mwandango. Moja ya vitu ambavyo ni lazima tuangalie ni uchomaji wa makaa. Hili jambo limekuwa kero kwa watu wengi kwa sababu wenye kuhifadhi misitu wanachukua nafasi ya kunyanyasa wale watu ambao wamechoma makaa. Ukishikwa na magunia saba, gunia moja tu ndilo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}