GET /api/v0.1/hansard/entries/616808/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 616808,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616808/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "litapatikana kama exhibit. Maofisa wa Serikali wanachukua hayo mengine na kuyatumia. Utakuta kwamba wao wenyewe ndio wanaendeleza hii biashara ya makaa kinyume na sheria. Ni ombi langu kwamba wakati huu tunahitaji kuhifadhi misitu. Tunataka kuhakikisha kuwa misitu imehifadhiwa. Kuna mpangilio mwafaka umewekwa kuhakikisha kuwa wale ambao wanashughulikia misitu wanafaidi kutoka hiyo misitu. Wale watu ambao wameamua kupanda na kuhifadhi miti binafsi, wataruhusiwa kupanda. Wakati wa kuivuna pia wapatiwe mpangilio vile wataivuna. La sivyo, tukiendelea hivi, utakuta hii nchi yetu imekuwa janga, ukame umeingia na hakuna chochote nchi hii itaweza kufaidi. Langu ni kuomba Wabunge wenzangu tuupitishe Mswada hii lakini tuangalie vile vipengele ambavyo vitasaidia mwananchi kuhakikisha kuwa misitu inayovunwa katika sehemu wanapotoka pia wao wenyewe wanapata faida. La sivyo, itakuwa vigumu sana sisi kuhifadhi hii misitu. Mchango wangu unakomea hapo. Ahsante."
}