GET /api/v0.1/hansard/entries/616863/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616863,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616863/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Naelewa kwamba Mswada huu pia utapelekwa kwa Bunge la Seneti na urudishwe hapa na, hivyo basi, tukakuwa na nafasi ya kuuzungumzia zaidi. Ningetaka tu kuwaunga mkono wenzangu waliozungumzia mambo ya kuhifadhi misitu. Katika Serikali ya Rais mstaafu mzee Moi, nilikuwa mwenyeketi wa KANU katika Wilaya ya Nakuru. Wakati huo, misitu yote ilikuwa imefungwa ili watu waweze kulima ndani. Niliweza kunyenyekea kwake na nikajua kitu kimoja. Hakuna wakati juhudi za kuhifadhi misitu zitafaulu bila ya kuwahusisha wananchi. Hapo mbeleni, uharibifu wa misitu ulikuwepo kwa sababu wananchi walifurushwa kutoka kwa misitu."
}