GET /api/v0.1/hansard/entries/616864/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616864,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616864/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Misitu haiwezi kulindwa kwa njia ya haki bila kuwahusisha wananchi. Ni lazima wafahamu kwamba misitu in mali yao na ni muhimu kuichunga. Siku hiyo nilipata nafasi hiyo na nikawa mtu wa kwanza - kabla nichaguliwe kuwa Mbunge - kurudisha mambo ya kulima ndani ya misitu. Imetufaidi sana kwa sababu Serikali haikuwa na pesa za kupanda miti na kulimia katika misitu. Wananchi wakihusishwa, itakuwa ni jambo rahisi sana. Hata sasa ni rahisi kwa sababu wananchi watapewa sehemu fulani ambako watalima. Kawaida, msitu hufukuza wakulima baada ya miaka mitatu kwa sababu miti ikifika miaka mitatu, hauwezi kupanda kitu kingine ndani. Kwa hivyo, tulijaribu sana."
}