GET /api/v0.1/hansard/entries/616865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 616865,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/616865/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Naunga mkono Mswada huu kwa sababu yale tunayoyazungumzia leo hii ni mambo nyeti ambayo tunastahili kusukuma ili yapite. Baada ya wananchi kulima na kupanda miti bila kulipwa, kuna mambo machache ambayo yataleta mabadiliko. Hii ni kwa sababu baada ya wananchi kuilinda miti hiyo, kuna shida ambazo zinawapata. Kuna watu kutoka Nairobi ambao hupewa vibali vinavyowaruhusu kuikata miti hiyo. Wananchi hao hawapewi hata kuni kutokana na mabaki baada ya miti kupasuliwa mbao licha ya kwamba wao ndio walioipanda miti hiyo. Uhusiano wa wakazi na misitu unaanza kuharibikia hapo. Wananchi wakikosa imani na kuona kwamba hawahusishwi kwenye juhudi za kuhifadhi misitu, uharibifu wa misitu unaanza. Lakini sheria ambayo tunaipendekeza hivi sasa itawawezesha wananchi ambao wanalinda misitu kupewa nafasi wakati wa kuvuna miti ili nao wafurahie. Serikali ikipata pesa kutokana na bidhaa za misitu, wananchi pia watafurahia kuni na malipo mengine."
}