GET /api/v0.1/hansard/entries/617337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 617337,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/617337/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Spika, naomba niunge Hoja hii mkono kwani Kamati hii ya Bunge, ni kamati muhimu inayotoa mipangilio yote ya Bunge na kuhakikisha kuwa shughuli za Bunge zinaendelezwa vilivyo. Ukiangalia orodha hii, tumeangalia kwa utaratibu tuone kama kuna wengine ambao hawashughuliki sana na shughuli za Bunge na wengine wakaamua kuwa hawangependelea kuendelea katika hivi vikao kwa sababu kila siku ya Jumanne wakati shughuli za Bunge zimemalizika, lazima Kamati hii iende ikutane na ijadiliane. Unakuta wakati mwingine, wanakamati wengine ambao wako katika orodha hii ama walikua katika orodha ya awali, hawakuwa wakishughulika na mambo ya Kamati. Hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa itakua ni jambo la busara kwa haya majina yabadilishwe. Hii ndio maana mwenzangu katika Hoja yake katika utangulizi wake, ameomba kuwa mabadiliko yawepo na tunaomba na kuwasihi Wabunge wenzangu wakubali hayo mabadiliko na orodha hii ambayo tumepeana iwe ndio tutakayokubalia iwe orodha ambayo itakuwa katika Kamati hii ambayo inashughulika sana na mambo ya Bunge."
}