GET /api/v0.1/hansard/entries/618135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 618135,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/618135/?format=api",
"text_counter": 323,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kunyonyesha mtoto wake na hivyo kuweka uhusiano wa karibu sana kati ya mzazi na mtoto na ndiposa dada zetu hupewa muda wa miezi mitatu baada ya kujifungua. Sheria inasema kwamba ikiwa mke atakwenda kwa miezi mitatu, mume atapewa wiki mbili. Lakini kwangu mimi, hivyo sio sawa. Namsihi Dada yangu, Sen.Wangari, aliyeleta Mswada huu, afikirie kwamba sio lazima mke apewe siku nyingi zaidi ya mume. Ikiwa uchungu wa mwana aujuaye ni mamaye, basi uchungu wa kulea mwana aujuaye ni mume. Mume ndiye anayetafuta chakula na hata kulipa kodi ya nyumba ili mtoto apate afueni ya kuishi katika maisha mema. Bw. Naibu Spika, mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Utendakazi na Maswala ya Kijamii, nilitembelea makao ya watoto yatima na nikajionea kwamba watoto hao ni wengi. Tukizingatia kwamba kuna Wakenya wengi ambao wanataka kuwachukua watoto hao na kuwalea---. Waswahili husema kwamba kuzaa si hoja, lakini kulea ndio uzazi. Nikizingatia swala hili, tunaona kwamba sheria zile zimewekwa za kueza kuchukuwa watoto kisheria zinahitaji kurekebishwa ili kuwapa fursa watu wasio na uwezo wa kupata mtoto kawaida, wawe na fursa nzuri ya kuweza kuwa na mtoto. Jukumu la kulea ni la wazazi wawili. Hatuwezi kusema kuwa jukumu la kulea ni la mama tu. Hata kipofu na walemavu pia wanaweza kuzaa lakini jukumu kubwa----"
}