GET /api/v0.1/hansard/entries/618171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 618171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/618171/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kunradhi dada yangu basi kama nimeongea jambo ambalo limekuguza moyo, sio sinto fahamu zangu. Utanisamehe. Bw. Naibu Spika, nilikuwa nasema ya kwamba katika Mswada huu ambao umeletwa na dada yetu Sen. Wangari, pia vilevile tumezingatia ya kwamba tumetangulia hapo awali kusema kuzaa sio hoja lakini kufuga ndio msemo ya kwamba ikiwa uko na uwezo wa kuzaa, basi uwe na uwezo wa kufuga. Ikiwa hauna uwezo wa kufuga, basi afadhali umpishe mwenzako ambaye ana uwezo wa kufuga. Kuna msemo usemao: “Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo”. Ule muda ambao mzazi anapewa kama ni miezi mitatu, uwe na mama awe na mtoto wake ndani ya nyumba, waweze kuzoeana na mzee pia akiwa pale pale. Hilo ni jambo ambalo tunataka kuzingatia katika vipengele hivi ambavyo tunataka kuvigeuza katika utendakazi wa sheria. Vile vile Bw. Naibu Spika, lazima tuzingatie kwamba kuna umuhimu wa likizo ya uzazi. Ikiwa likizo ya uzazi haitalingamana, mimi nimetangulia hapo awali kusema ya kwamba likizo ya uzazi ianze kuhesabiwe zaidi. Tunajua kuna mwezi mmoja ule mtu anaweza kuenda katika likizo ya uzazi ili apimwe na mambo kama haya. Wakati muda ule unaendelea, tusiuhesabu. Sheria husema ya kwamba wakati mama amezaa, ndipo likizo ya uzazi huanza kuhesabiwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}