GET /api/v0.1/hansard/entries/618308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 618308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/618308/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Hii ndio maana Kiongozi wa walio wengi Bungeni anapendekeza kuwa yule ambaye ameleta Hoja apatiwe dakika sitini na Wabunge wengine wapatiwe dakika kumi kutoa michango yao kwa Hoja hii. Ninaomba pia ieleweke kuwa litakuwa jambo ambalo limekwisha changiwa katika Kamati za Bunge na Wabunge wakatoa maoni na mapendekezo yao na lile ambalo litaletwa hapa Bungeni ni jambo ambalo lishakubalika. Hapo ndipo Wabunge watapata nafasi ama ruhusa ya kulichangia na kuweka msimamo kuhusu jambo hilo."
}