GET /api/v0.1/hansard/entries/618423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 618423,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/618423/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Wenzangu wa upande ule wa pili walikuwa wananiita niende upande ule lakini Wakenya wangeona nimewasaliti na ikawa ni bora nikae huku. Ninakubaliana na utaratibu wa mwendo ambao umeletwa, kwa lugha maarufu ya Kiingereza “ Procedural Motion”, ili kuweka muda wa ambao utahakikisha kila mmoja ananafasi ya kujadili na kutoa maoni yake katika maswala haya. Hili ni jambo ambalo halitasaidia Bunge hili peke yake, lakini pia litaweza kusaidia Wabunge wajao watakaokaa katika viti vivi hivi na watakaozingirwa na kuta zizi hizi. Wengi wameyazungumzia mambo haya. Ninaomba unipatie fursa na wenzangu wanipatie fursa nitaje hili swala. Kila mmoja wetu alipokuwa anaomba kura na kuzungumza katika mashinani, tulikuwa tuna mrengo fulani ambao tulikuwa tunafuata. Sisi wana CORD tunaamini ule mrengo, ndio njia mwafaka ya kuendesha hii nchi. Yamezungumzwa mengi kuwa watu wakiwa wametolewa katika kamati fulani, itakuwa wamefanyiwa dhambi. Lakini lile tunalisahau ni kwa njia ile dhambi inavyofanyiwa wale Wakenya wote wengine waliobaki. Hii ni kwa sababu, ikiwa utakuwa ni mwenye kuingia katika kamati fulani na mawazo yako na maoni yako hayalingani na yale matakwa ya Wakenya waliokupigia kura--- Hii ni kwa sababu waliokupigia kura walifanya hivyo kwa minajili ya ile"
}