GET /api/v0.1/hansard/entries/619705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 619705,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/619705/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Asante sana Mheshimiwa Spika. Hii Ripoti inaonyesha wazi kuwa watu hutumia sukari kufanya mifuko yao iwe mitamu. Ninataka kuwakumbusha kwamba kuna baadhi ya Wabunge walitaja kuwa mambo ya sukari ni ya kwao, lakini kwa hekima za wakoloni, kiwanda cha kwanza kilianzishwa Kenya mnamo mwaka wa 1922 katika sehemu ya Miwani. Kiwanda cha pili kilikuwa Pwani mnamo mwaka wa 1927 kule Ramisi. Serikali zote ambazo zimepita zimedharau sekta hii. Ni hamu yetu kuwa tutaweza kuiinua sekta hii. Hii Ripoti ililetwa katika Bunge mwezi wa Machi mwaka wa 2015. Ilipoletwa, Kenya ilikuwa na pazia ya kujisitiri na sheria za COMESA. Hizo sheria zikawa zinasitiri Wakenya kuwa hakuna sukari itakayoingia mpaka mwezi wa Februari mwaka wa 2016 na tayari tumeipita. Ndiyo maana kila siku mimi husema kwamba kuna haja ya kila tunachokizungumzia ama tunachokifanya tuangalie na tujue kwamba kuna wenzetu katika sehemu nyingine ulimwenguni ambao wanafanya mambo yao pia. Tunajadili Ripoti hizi zikiwa zimepitwa na wakati. Ninawaomba Wabunge wenzangu waniazime maskio yao. Mwaka wa 2015, Baraza la Mawaziri liliidhinisha ubinafsishaji wa viwanda vyote vitano vya sukari ambavyo vinamilikiwa na Serikali ya Kenya. Mimi ni Mwanachama wa Kamati inayohusika na masuala ya fedha. Katika mwezi wa Aprili, 2005, Bunge hili lilipitisha Hoja ambayo ilisema kwamba kabla ya viwanda hivyo kubinafsishwa, ni lazima Serikali ilete Miswada ya uwiano na serikali za Kaunti ili tujue kwamba tunaweza kubinafsisha viwanda hivyo bila wakulima kupoteza raslimali zao. Simuoni Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na masuala ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Sitaki kuifanya hii kuwa hoja, lakini ninawaomba wahusika waangalie iwapo kulikuwa na makosa walipokuwa wakichapisha Ripoti hii. Wao wameandika kwamba Bunge hili lilipitisha Mswada huu Februari, 2013, lakini Hoja hiyo ilipitishwa katika Bunge na Kamati inayohusika na Fedha, ambayo mimi ni mmoja wao mnamo Aprili, 2015. Ninaomba, Mhe. Spika ukumbuke jambo hili. Tunapojikumbusha pia tunaikumbusha Serikali umuhimu wa sekta ya sukari. Miwa nchini Kenya inakuzwa kwenye ardhi ya hektari 2,000. Zaidi ya wakenya laki tatu ni wakulima wa miwa. Sekta ya sukari kwa njia moja au nyingine inatoa ajira kwa Wakenya milioni sita. Idadi hii ni asilimia 16 ya Wakenya wote. Hii si idadi ndogo. Sekta ya sukari inachangia uchumi wa Kenya kwa kiasi cha asilimia 7.5. Ndio maana tunasisitiza kwamba Serikali ilete sheria inayoambatana na Hoja iliyoletwa hapa na Kamati inayohusika na masuala ya fedha na kupitishwa na Bunge hili. Tunataka sheria ipitishwe na Bunge hili ili wakulima wasidhoofike."
}