GET /api/v0.1/hansard/entries/619707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 619707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/619707/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Colombia inaweza kutoa tani 115 za sukari ilhali nchini Kenya hektari moja ya miwa inatoa tani 60.5 za sukari pekee. Ni lazima pia tujiulize ni kwa nini gharama ya kukuza miwa nchini Kenya ni US$ 2.5 kwa kila tani ya sukari ilhali katika nchi jirani gharama hiyo ni US$13 pekee kwa kila tani ya sukari. Ni lazima pia tujue ni kwa nini gharama ya kusaga sukari nchini Kenya ni US$700 kwa kila tani kwa mkulima ambaye hakuchukua mkopo kutoka kwa benki na US$870 kwa kila tani kwa mkulima ambaye amechukua mkopo kutoka kwa benki ilhali nchini Malawi gharama hiyo ni US$350 kwa kila tani, nchini Zambia ni US$400 na nchini Brazil ni US$300 pekee. Mambo haya hayawezi kufanywa na mtu binafsi, awe ni Mbunge ama mtu mwingine yeyote. Serikali ndiyo yenye uwezo na wadhifa wa kuangazia masuala hayo. Ningependa kuelezea tena umuhimu wa Serikali kuwa na mshikamano. Kuna ripoti ambayo ilichapishwa katika mwaka wa 2013/2014. Kila mtu anaweza kuipata na kuisoma ripoti hiyo. Kulingana na ripoti hiyo, tani 15,140.4 ziliingizwa humu nchini na kutumiwa na wakenya. Sukari hiyo ililetwa kutoka sehemu tofauti za ulimwengu. Bodi ya Sukari Nchini (KSB) haikuidhinisha kuingizwa kwa sukari hiyo nchini Kenya. Wamiliki wa kampuni tano pekee ndio walionufaika kutokana na mauzo ya sukari hiyo ilhali Wakenya wengine wakilalamika tu na kuishi katika hali ya uchungu kama shubiri. Hadi leo, hakuna mtu hata mmoja katika halmashauri ya ushuru nchini ambaye amechukuliwa hatua ya kisheria na kupelekwa mahakamani kwa sababu ya sakata hiyo. Hili suala liliangaziwa na Kamati hii. Suala hilo lilijadiliwa kwa kina na ushahidi kwamba tani 15,140.4 za sukari ziliingizwa humu nchini katika mwaka wa 2013/2014. Ningependa kuipongeza Kamati yetu inayohusika na ukulima kwa kazi njema waliofanya. Ninaomba tena upande wa Serikali uwe mchangamfu. Suluhisho la kuboresha sekta ya sukari nchini si kufurahisha Wabunge ama watu wengine kwa kusema kuwa watatoa billioni moja kwa kiwanda kinachoanguka. Suluhisho ni kuangalia mambo haya ili kesho tusirudie kusema kwamba Wakenya wanapoteza pesa zao. Hilo ndilo suluhisho, na haya ndio matakwa ya Wakenya, ambayo tunafaa kuyazungumzia hapa Bungeni."
}