GET /api/v0.1/hansard/entries/620585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620585,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620585/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninataka kutoa pongezi kwa Mswada huu ambao umeletwa katika Bunge. Huu ni Mswada ambao unatekeleza masharti ya Katiba ya Kenya kulingana na vipengele 19(2), 48, 50(2)(g) na (h). Katiba ya Kenya inaeleza wazi kuwa kila Mkenya ana haki ya kupatiwa msaada katika masuala ya kisheria. Pia, ni muhimu Serikali iweke jopo litakalosaidia wasiojiweza katika masuala yanayohusiana na mahakama. Historia ya Kenya inaelezea wazi wakenya wamefungwa kwa muda wa miaka, na wote kwa sababu wamekosa uwakilishi katika mahakama. Ukiangalia watoto na akina mama utakuta kwamba wamepata dhuluma za aina tofauti kwa sababu hawana watu wa kuwawakilisha katika mahakama. Kama vile wenzangu wamezungumza, tunaukubali na kuunga mkono Mswada huu ili tutekeleze masharti ambayo yako katika Katiba. Lile tu ambalo tunataka kulieleza ni kama Kenya inataka kusonga mbele tusiwe watu wa kuyazungumza mambo leo kisha tunaanza kuyajadili tena na inachukua muda kuyatekeleza. Tunaomba kwamba katika Bajeti ya mwaka huu, fedha za hii kamati zianze kutengwa kuanzia sasa ili watu wafaidika kutokana na masuala ya kisheria. Kuna mashirika ambayo yamejitolea kusaidia akina mama, vijana na hususan kupigania haki za kibinadamu. Pia, mtu anapodhulumiwa katika mahakama mashirika haya yamejitokeza na kuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za huyo mtu. Ni muhimu ikiwa Serikali itaunda jopo hili na kutenga fedha hizi ili zisaidie mashirika kama haya yasiangamie bali yaendelee na kazi zile. Pia, kuna umuhimu wa jopo la mawakili ambao watawekwa katika sekta hii wawe katika kila kaunti. Wasiwe ni watu wa kusumbua. Kwa mfano, mtu akihukumiwa na anahitaji usaidizi katika kaunti ya Kilifi ni lazima afike Mombasa ilia pate usaidizi, ama mtu anahitaji usaidizi Mombasa lakini mpaka afike Nairobi ndio apate usaidizi. Tukifanya hivi tutakuwa tunaenda kinyume na vile Katiba inavyozungumza. Vile vile kuna kipengele kinazungumzia vile ile bodi itakavyokuwa. Ni nani atakaa katika hii bodi? Mwenyekiti wa bodi hii atachaguliwa na Rais wa Kenya. Ningeonelea, na nina imani kuwa ni fikira za wenzangu pia. Ili kuimarisha demokrasia katika Kenya, tuko na mkono wa Serikali ambao ni urais na Baraza la Mawaziri, mahakama na wale wenye kuangalia na kutunga sheria yani Mabunge mawili - Bunge letu na Bunge la Seneti. Kwa hivyo, ninaonelea kuwa Rais asiingilia jopo hili, bali aliache lihusike na maswala ya mahakama. Isiwe kuwa kuna mkono wa inje ambao unaingilia mambo haya. Pia, bodi hii imetaja watu tofauti tofauti kuanzia kipengele cha 9(a) mpaka (o). Ukiangalia kwa kina, utakuta kwamba wengi ni wawakilishi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}