GET /api/v0.1/hansard/entries/620620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 620620,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620620/?format=api",
"text_counter": 344,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Katika afisi yangu, ninakutana na watu wengi sana. Kwa mfano, Rockerfeller Okeyo, ambaye ni mlemavu, alifanya kazi katika shule moja kule Asumbi na wakati pesa zilipotea akiwa mhasibu wa shule, akazingiziwa ilhali yeye ni mlemavu na watu walikuwa wamevunja ufa na kuingia kule ndani. Amefuatilia ile kesi lakini amekuwa na mawakili matapeli ambao wanahongwa na mwishowe wanamuachia ile kazi. Mwishowe, kumekuwa na kesi ya mama mwingine anayeitwa Lucy Wangeci, ambaye ako na ulemavu wa kutokuona. Ameachiwa shamba kubwa kule Kirinyaga lakini kwa sababu yeye hajaolewa kwa sababu ya ulemavu wake, ananyimwa lile shamba na linauzwa na ndugu yake na hana afueni. Hapati hata mtu wa kumwakilisha. Nakumbushwa pia kuhusu Tabitha Wairimu ambaye mtoto wake, Kuria, aliuawa kupitia ajali ya barabarani lakini bado anafuata kesi hii kwa sababu wakili ameshakula pesa baada ya kulipwa na ile kampuni ya bima. Yeye hajawahi kupata haki yake. Kuna mambo mengi tu ambayo yamewasomba watu wetu wakitafuta haki yao lakini hususan hawawezi wakapata msaada wa kisheria wa uwakilishaji. Mwishowe, wanaendelea kutokota katika biwi la umaskini na simanzi."
}