GET /api/v0.1/hansard/entries/620623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620623/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Ninapoangalia Mswada huu, naweza kuupigia upato zaidi na niseme kongole kwa wale wameufikiria kwa muda mrefu. Mwanzo, Mswada huu umetoa mkakati ambao unafaa kufuatiliwa wakati tunatafuta watu ambao watatetea maskini. Mwanzo, kuna mfuko wa fedha ambao umetengwa lakini ningependa kusema kuwa ni jukumu la Bunge hili kuhakikisha kwamba pesa za kutosha zimetengwa mle kwa sababu ile ada ambayo inatozwa na mawikili ni ya bei ghali mno. Nikiuangalia huu Mswada, naona ile huduma ya kuwapatia Wakenya huduma za kisheria bure inaweza kutoa ada fulani. Lakini ningependa kusema kwamba hilo ni jambo ambalo tunafaa kuliangazia kwa sababu ukiseme kwamba ni lazima yule ambaye anafaa kusaidiwa alipishwe pesa, inamaanisha pia hicho ni kikwazo kingine. Watu wengine, hata kupata shilingi mia moja jameni, hata ile nauli ya kwenda katika zile afisi itakuwa ni mhali sana. Kwa hivyo, ningependa kusema kwamba tusiweke vipengele katika sheria ambavyo vitakuwa vyenyewe ni vikwazo kwa wale ambao tunajua kwa kweli hawana uwezo. Watu wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku katika nchi hii. Kama mtetezi wa wanyonge, ningependa kusema kwamba tusiangazie tu kwamba eti kwa sababu unataka kuwa mtu aweze kujihuzisha na kesi ya kwake, ni lazima atoe hela. Wakijitolea, waje, watoe malalamishi yao, basi litakuwa jambo la muhimu. Pendekezo katika sheria hii ni nzuri sana kwa sababu kuna uwakilishwaji wa hali ya juu sana wa mashirika tofauti na watu tofauti tofauti. Kwa mfano, ninafurahi kuona kwamba kuna ile Tume ya Haki za Kibinadam, Kenya National Commission on Human Rights. Pia, kuna ile halmashauri ama Baraza la Kitaifa Kuhusu watu wenye Ulemavu; National Council for Persons with Disabilities. Lakini ningependa kuunga mkono kwamba ingalikuwa ni muhimu pia kuwa na masuala ya jinsia na vijana, kwa sababu hao ndio wanapata dhuluma kila wakati na unyanyasaji, pia, tungehakikisha kwamba hii sheria inawiana na ile nyingine ya Victim Protection, kwamba waadhiriwa waweze kulindwa. Mara nyingi, wale ambao pia watahitaji msaada ule wanaweza kuwa ni watu ambao wamedhulumiwa kwa njia moja ama nyingine. Kwa hivyo, kama kungeweza kuwa na uwakilishaji ambao unafaa, basi ingelikuwa ni mhimu. Pia, swala sugu ambalo linajitokeza ni kuwa ni nani atakayekuwa mhusika wa jambo hili. Mwanasheria Mkuu ama Afisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikari na Katibu mhusika, wawe ndio wanaangazia shirika la huduma hizi za kisheria ndiposa kusiwe kuna mwanya katika Serikali kuhusu ni nani anayefaa kuwa akipata hizi ripoti. Pia, kuna changamoto nyingine kuhusu ada za wanasheria ambao watahusika. Najua wenzangu wamezungumzia kuhusu kuwa pengine watu wengine watapendelewa kupata hizi kazi zote. Hilo ni jambo ambalo linafaa kuangaliwa katika kanuni za sheria hii, isiwe kuna watu ambao wanapendelewa. Fauka ya hayo ni kuhakikisha kwamba kila wakati ambapo swala hili linazungumziwa, ukipeleka kesi kortini, hizo ada zifuatiliwe na ziwekwe vizuri kwa wino ambao unaonekana ndiposa tusianze kupata habari kuwa kuna wakili fulani ambaye alimwakilisha Isaac Mwaura, Tabitha Wairimu ama Rockfeller Okeyo halafu mwishiwe anaitisha mamilioni ya fedha ambazo haziwezi kulipwa na Serikali. Tunafaa kuhakikisha kwamba hakuna utapeli wa pesa za Serilaki iwe kwamba watu wanawapatia wengine hela ndiposa waweze kupata mlungula, chai au The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}