GET /api/v0.1/hansard/entries/620649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 620649,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620649/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Kwa hivyo, tukiwa na mawakili ambao wanalipwa na Serikali itawasaidia sana wale walalahoi nchini kwetu ili kupata msaada, hususan wale ambao wanadhulumiwa kiasi kama hicho na zaidi. Kwa mfano, pia, kuna wanawake wengi Kwale ambao mara kwa mara wanakuja kwa sisi viongozi wakitaka msaada kuwatoa vijana wao ambao wameshikwa na wamefungwa gerezani na hawajui vipi watawatetea watoto wao. Wengi ambao wanashikwa huwa ni vijana wa kiume kwa bahati mbaya na afisa wetu wa polisi kwa maswala ambayo hayaeleweki mara nyingi, katika mambo ambayo tunayaita misako. Maafisa wa polisi wakimpata kijana anatembea tu, wanamshika. Wakati mwingine wanamua kwa muda kushika watu ama kuingia kwa nyumba za watu na kushika vijana bila hatia yoyote. Halafu kina mama ndio wanaumia kwa sababu hawawezi kuwatetea vijana wao."
}