GET /api/v0.1/hansard/entries/620652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620652/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Jambo nzuri katika sheria hii ni kuwa watu ambao hawana nchi ama kwa Kiingereza “stateless persons”, wataweza kupata msaada wa mawakili ili kusaidika katika kesi zao tofauti tofauti. Pia, ingekuwa vizuri kama wangeweza kupata msaada ili kuwatetea pia wao waweze kutambulika kama Wakenya. Makonde hapa nchini wako kama 10,000, watu wengi sana ambao wanaumia na wameoana na Wakenya hapa nchini. Watoto wao wanapata shida wakitaka kuandika karatasi za usajili wa kuzaliwa, kupata vitambulisho au hati za kusafiria kwa sababu pengine mzazi wao mmoja hatambuliki kama Mkenya. Kabla sijaketi, ningetaka kuiomba, kwa sababu nina hakika hii sheria itapita katika muda usio mwingi, Serikali ifuate maelezo ya sheria hii ili isiwe kama ile Sheria ya Baraza la Vijana la Kitaifa, ambayo Serikali imekataa kutaimbua na kuwapatia vijana pesa ili waweze kuendeleza maswala yao kama vile walivyoruhusiwa na Sheria ya Baraza la Vijana la Kitaifa ya 2009. Kwa hayo machache, nasema shukrani."
}