GET /api/v0.1/hansard/entries/620811/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 620811,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620811/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Walemavu katika nchi yetu ya Kenya ni takriban asilimia 15. Hawa wanaishi na ulemavu tofauti tofauti. Pia, tuzingatie ya kwamba ulemavu ni kwa njia nyingi. Wengine wana ulemavu wa macho, wengine wana ulemavu wa masikio na wengine wana ulemavu wa vyungo tofauti tofauti. Katika Katiba yetu ya Kenya, katika kifungu cha 54(c) kinazungumzia umuhimu wa kuwezesha walemavu waweze kutembelea maeneo tofauti tofauti bila matatizo, waweze kupata usafiri bila kuwa na matatizo na pia waweze kupata habari au kupashwa habari bila kuwa na matatizo. Jambo hili haswa la habari naona ni changamoto kubwa sana. Lakini najua Mhe. Mwaura pia ana Mswada ambao haujafika Bunge hili lakini utafuka ambao utazungumzia hasa masuala ya upasaji habari kwa sababu mpaka sasa tunaona vyombo vyetu vya habari havijatimiza sheria ya kushirikiana na walemavu kupata habari kimwafaka."
}