GET /api/v0.1/hansard/entries/620814/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620814,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620814/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Tukiangalia majengo yetu mengi haswa ya umma hayajazingatia suala kama hili. Katika benki zetu, hospitali na mahoteli yahajazingatia haya. Hivi karibuni nilikuwa na Mhe. Sen. Godliver katika warsha ya Kamati ya Bunge. Tulipelekwa kwa hoteli moja ambayo inaitwa Medina. Ilibidi tukose kufanya warsha ile kwa siku ya kwanza kwa sababu ukumbi wa mazungumzo ulikuwa umewekwa katika gorofa nambari nne na ilikuwa ni ngazi pekee na kulikuwa hakuna lifti. Basi ilibidi Seneta aweze kuteta sana mpaka ikabidi tuache kufanya warsha hiyo tukasema tuifanye siku ya pili. Ilitubidi tuifanyie nje ya hoteli. Hatukuifanyia kwa ukumbi wowote. Hivo basi hata sisi katika Bunge hili, wakati tunaenda kupanga mikutano ya Wabunge, lazima tujue tuna Wabunge wenzetu na Maseneta wenzetu ambao wana hali ya ulemavu. Mbali na mijengo, tunaona walemavu ambao wanatumia yale magari yao ambayo imetengenezwa kuwabeba lakini hakuna pahali pa kuegesha magari kama haya. Wakati wanataka kuegesha vigari vyao, kunakuwa ni hali ngumu sana. Hivyo basi, swala hili ni lazima lizingatiwe."
}