GET /api/v0.1/hansard/entries/620818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620818,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620818/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Watoto wetu wengi, haswa wale ambao hawasikii na wale walemavu wa macho wameshindwa kuona alama za barabara na kwenye majengo. Kunatumika alama za kuonyesha ya kwamba ikiwa unaenda huku unafuata upande fulani. Wakati alama na ishara hizo zinatengezwa hutambulika ya kwamba kuna wenzetu walemavu ambao hawataweza kusoma ama kuzitambua kama vile sisi tunavyoweza kuzitambua. Tunajua tumepata majanga mengi sana hapa nchini kwetu Kenya kutokana na matatizo haya ya kuwa tumeacha kuzingatia walemavu. Walemavu wengi huishia katika majengo ambayo pengine kumetokea moto. Anataka kukimbia atetee roho yake lakini unapata kwamba kutokana na majengo yalivyojengwa, mlemavu kama huyu atabakia pale kwenye kiti chake ama pengine yule ambaye anatumia magongo abaki kwenye magongo yake na apatikane na athari kama hiyo. Tujitayarishe kwa haya mambo ya majanga kama Wakenya ili yanapotokea tujue watu walioko pale jinsi watakavyoweza kusaidika. Tuweke katika akili zetu na tutie maanani kwamba kila mahali katika umma kuna walemavu ambao wanatembea mahali pale na chochote kinaweza kutokea na wakati kimetokea, je hao watasaidika kwa njia gani? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}