GET /api/v0.1/hansard/entries/620819/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 620819,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/620819/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Sisi kama viongozi wa taifa hili la Kenya tunataka tuwe msitari wa mbele kuhakikisha kwamba sheria hizi kweli zimetekelezwa kwa sababu mara nyingi sheria tunazitunga na zinakuwa pale tu kama sheria. Mtekelezaji ni nani na ni nani atakayehimiza sheria zitekelezwe ikiwa kutakuwa hakuna watu wa kuhimiza sheria na kuweka msukumo thabiti wa kuhakikisha kwamba walemavu wana haki kama Mkenya mwingine yeyote? Walemavu hawatachukuliwa tu kwa sababu tumeingia katika mikataba ya kiulimwengu ama kwa sababu Katiba imependekeza hivyo basi sisi tunafanya tu kama kuonyesha. Ni lazima iwe ni haki yao ya kimsingi na ni jambo ambalo litafanywa kwa mikataba vile inavyotakikana. Iwapo yeyote atakiuka, sheria lazima itamfuata. Kwa hayo mengi ama machache, nataka kutoa kongole tena kwa Hoja hii. Ninamhimiza Mhe. Mwaura alete Mswada Bungeni ili tuuchangia na tuwe na sheria kabambe na mwafaka ya kuwalinda ndugu zetu walemavu. Asante, Mhe. Naibu Speaker wa Muda."
}