GET /api/v0.1/hansard/entries/62088/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 62088,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/62088/?format=api",
    "text_counter": 277,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nichukue nafasi hii nitoe mchango wangu juu ya Hoja hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Bw. Ogindo kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni Katiba yetu ya sasa inatupa nafasi ya kuelezana mambo kwa uwazi. Huu ni uwazi wa makadirio ya pesa na shughuli za Serikali kwa jumla. Mara nyingi makadirio ya pesa za Serikali yanaficha mambo mengi. Hoja hii inalenga madeni ya Serikali yetu na kutaka yawekwe wazi. Kwa nini Serikali inaona shida kuwaambia Wakenya kuwa kabla tupate Uhuru kulikuwa na madeni haya, na tangu tupate Uhuru tumekuwa na madeni haya mpaka siku hii ya leo? Wakati mwingine Kamati inayohusika na matumizi ya pesa za Serikali hapa Bungeni humwalika Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha kuja mbele yake ili aeleze juu ya deni letu. Yeye huona vigumu kuja mbele ya Kamati na kueleze wamekopa kiasi gani cha pesa. Inakuwa ni vuta ni kuvute. Hoja hii inaipa nafasi Bunge kumshurutisha Waziri wa Fedha kufika mbele ya Bunge na kueleza mengi kuhusu deni la Serikali. Ni lazima aeleze kinagaubaga deni la Serikali."
}