GET /api/v0.1/hansard/entries/62090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 62090,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/62090/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba pia niaangazie haya ambayo yamesemwa na wenzangu kuhusu mikopo iliyochukuliwa na mashirika kama Kampuni ya utengenezaji wa mbolea; Ken-Ren Chemical and Fertilizers Company Limited. Mkopo huu ulichukuliwa wengine wetu walipokuwa shuleni. Pesa hizo zilienda wapi? Hakuna mtu yeyote analifahamu jambo hili na mpaka sasa tunaambiwa tulipe pesa hizo. Waliokopa pesa hizo ni akina nani? Je, ni ukweli Serikali haijui ni akina nani waliyokopa pesa hizo? Kuna mtambo wa nyama ambao ulikuwa unajengwa huko Ngong uliojulikana kama Halal Meat Farm Factory. Mpaka leo, tunalipa mkopo uliyochukuliwa kujenga mtambo huo. Ni jambo la aibu kuwa tunalipa pesa hizo na hakuna mtu anayejua wanaolipwa ni akina nani. Katika lugha ya Kingereza mtambo huu kwa sasa ni âwhite elephant projectâ. Miradi kama hiyo ni mingi nchini, na tunaendelea kulipa deni za Serikali. Pesa hizo zinalipwa akina nani? Barabara ya Voi hadi Taveta ni mbaya muno. Makadirio ya Serikali ya 1960s hadi 1970s inaonyesha pesa nyingi zilitengewa barabara hii. Pesa nyingi zilikopwa kutoka kwa mataifa wafadhili na barabara hii ikatengenezwa. Barabara yenyewe haina lami. Ni aibu iliyoje kuwa mkopo huo unalipwa hadi sasa! Bw. Naibu Spika wa Muda, kama wenzangu walivyosema, wakati tulipokuwa tunapata Uhuru, kuna Wazungu na Wahindi walioondoka kutoka hapa nchini. Kulingana na haki zao, ilikuwa wawe wakilipwa marupurupu ya kustaafu lakini wanaendelea kulipwa hadi sasa. Wajane wao wanaendelea kulipwa. Ukiomba orodha ya watu wanaolipwa huko Uingereza, huwezi kuipata. Je, watu wanaolipwa pesa hizo ni akina nani? Kwani ukiwa unadai deni, mbona usimtambue na useme fulani ana deni langu? Alinikopa pesa fulani na ndio sababu ninamlipa. Mpaka leo hakuna hata mmoja anayetambulika kama yuko hai au amefariki lakini hizo pesa zinalipwa. Hoja hii ni mhimu kwetu wakati huu ambao tunataka tuanze maisha mapya kuambatana na Katiba mpya. Tunataka kila kitu kiwe wazi. Tunataka tuwajue wale waliokopeshwa pesa au walikopa pesa. Tunataka tujue tulikopa pesa kutoka kwa akina nani. Tunataka kujua ni akina nani walifanya miradi ambayo ilikuwa ya Serikali wakati huo na kadhalika. Kila mara Waziri wa Fedha huja hapa na kusema ni lazima tulipe pesa hizi. Wabunge huulizwa kupitisha Hoja na Miswada ya kuhakikisha pesa hizi zimelipwa bila kuuliza maswali mengi. Inakuwa ni lazima zilipwe. Wakati umefika mambo haya yote yawekwe uwazi. Ni lazima wananchi wetu wajue deni la Serikali na ni akina nani wanalipwa pesa hizo. Tuelezwe wazi wazi pesa hizi zilikopwa kufanya mradi fulani na kadhalika; tumekopa hapa na tumelipa kiasi hiki na kile. Haya yote yanakuwa ni shida kueleza. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache ninaunga mkono."
}