GET /api/v0.1/hansard/entries/621351/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 621351,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/621351/?format=api",
"text_counter": 337,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "namshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Sen. (Dr.) Kuti, kwa kuleta Mswada huu wa kurekebisha vipengele vya sheria ili kusaidia kupigana na maradhi ya saratani. Bw. Spika wa Muda, jambo hili ambalo limeletwa ni mwafaka. Miaka michache iliyopita, Wakenya wengi hawakujua kuwa maradhi ya saratani huuwa. Hawakujua kuwa maradhi haya humshika mtu kulingana na vile anavyoishi na vyakula vya kisasa anavyokula. Kwa hivyo, lingekuwa jambo mwafaka Serikali kuu na Rais wa Kenya, kutangaza hili kuwa janga la kitaifa ili Wakenya wote tufahamu kuwa ikiwa ni janga la kitaifa, pesa zitawekwa na wafadhili wataingilia maswala haya ili kusaidia wananchi kutokana na ugonjwa wa saratani. Sijui kama Wizara ya Afya ina takwimu ya idadi ya wananchi wanaokufa kila siku au kila mwezi kutokana na maradhi ya saratani kwa sababu ni wengi. Kila wakati, tunafanya michango ya kutuma watu wetu kwenda India kusaidiwa huko kwa vile India inajulikana kuwa na umaarufu wa kutibu maradhi mengi. Hata hivyo, tunapowatuma huko, huwa wamefikia kiwango cha mwisho ambayo ni Stage Four . Linakuwa janga la kifamilia na kitaifa---"
}