GET /api/v0.1/hansard/entries/621356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 621356,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/621356/?format=api",
"text_counter": 342,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okong’o",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 948,
"legal_name": "Kennedy Mong'are Okong'o",
"slug": "kennedy-mongare-okongo"
},
"content": "Nashukuru, Bw. Spika wa Muda. Bw. Spika wa Muda, nilikuwa nasema kwamba wananchi wa Kenya wameathirika sana jinsi ilivyosemwa kwa vile hakuna elimu ya kutosha, hakuna vifaa vya kutosha na wataalamu wa kutosha. Ninapounga mkono pendekezo hili la kubadilisha sheria, Serikali kuu ikishirikiana na Serikali za kaunti inafaa kulipa jambo hili kipaumbele ndiposa wananchi waweze kushughulikiwa na kusaidiwa kutokana na maradhi haya. Nimesema kuwa ni jambo la umuhimu Serikali kuu ama Rais wa Kenya kulitaja kuwa janga la kitaifa. Nimeangalia mapendekezo kadhaa wa kadhaa ambayo yamewekwa hapa. Tutaangalia mapendekezo machache ambayo yatarekebishwa wakati tutakapokuwa tukijadili Mswada huu. Bw. Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono."
}