GET /api/v0.1/hansard/entries/621901/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 621901,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/621901/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwa wakenya ama ni mambo la kubahatisha kwa sababu ikiwa askari wetu anaweza kupigwa, na kila mtu nchini akaweza kuona katika runinga? Bw. Spika, je, kama yule askari angekuwa mwanaume, angeweza kufanya kitendo kama hicho? La! Kama angekuwa kibonge kama ndugu yangu Sen. Karaba, je angeweza kufanya kitendo kile? Wangepambana pale pale. Lakini alichukua nafasi hiyo kwa sababu aliona ya kwamba yule ni mama ambaye hana uwezo. Sisi tunashtumu kitendo hicho sana kwa sababu ni kitendo cha dharau kwa Wakenya wote. Ni kitendo ambacho hakifai kufanywa na mtu yeyote hapa nchini. Licha kwamba kimefanywa na mtu ambaye tunamuona rangi yake ikiwa ni tofauti, hatujali kama yeye ni Mkenya au la. Jambo la muhimu ni kuwa sheria lazima ifuate mkondo wake. Huyu mtu ashikwe, apelekwe ndani na aweze kufunguliwa mashtaka mara moja. Tunataka kuona ni Jaji yupi atakayechukua kesi hiyo kama atamwaachilia au kumhukumu. Hii ni kwa sababu Wakenya wote waliona kitendo hicho cha dharau kikifanyika wazi. Huyu ni mtu wa kufungiwa korokoroni. Ikiwa si mwananchi wa Kenya, sheria pia inasema kwamba achukuliwe hatua na afungwe vile vile. Hatutaki kuona mabalozi wakiingilia kesi hii kwa sababu kitendo hiki cha dharau kimetendeka. Bw. Naibu Spika, kitendo kama hiki kiliwahi kufanyika miaka mingi iliyopita. Tulishuhudia kitendo kama hicho katika Pwani. Dada zetu walikuwa wakifanya biashara katika ufuo wa bahari na mtalii mmoja aliyejifanya askari akamuua dada mmoja. Hatimaye, kesi hii haikuchuliwa kwa uzito. Mabalozi mbalimbali waliingilia kati na mtalii huyo akaachiliwa huru. Kwa hiyo, katika kesi hii ni lazima askari wetu wafanye kazi bila kuingiliwa kati na mtu au ubalozi fulani. Ikiwa sheria hii inaweza kutumika kwa Mkenya, wembe ni ule ule. Ni lazima huyu jambazi aliyefanya kitendo hicho achukuliwe hatua mara moja."
}