GET /api/v0.1/hansard/entries/622206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 622206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/622206/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "UTILIZATION OF BUKHAYO CENTRAL WARD DEVELOPMENT FUND Hili ni ombi la wakaaji wa Wadi ya Bukhayo ya Kati katika Kaunti ya Busia kuhusu matumizi ya fedha zilizotengwa kupitia Hazina ya Maendeleo ya Wadi (WardDevelopment Fund) na Serikali ya Kaunti ya Busia katika Mwaka wa Kifedha 2014/2015. Maseneta Waheshimiwa, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge la Seneti, Vipengele Nambari 220(1)(a) na 225(2)(b) ninatoa taarifa kwa Seneti kwamba dua limewasiliswa, kupitia kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge la Seneti, na wakaaji wa Wadi ya Bukhayo ya Kati katika Kaunti ya Busia kuhusu matumizi ya fedha zilizotengwa kupitia Hazina ya Maendeleo ya Wadi (Ward Development Fund) na Serikali ya Kaunti ya Busia katika Mwaka wa Kifedha 2014/2015. Katika dua lao, wakaaji hawa wanaomba msaada wa Bunge la Seneti ili kubaini ukweli na kupata haki kuhusu miradi ya maendeleo iliyopaswa kutekelezwa katika wadi hiyo katika Mwaka ambao umetajwa, na ambao utekelezwaji wake aidha haukufanyika ama ulifanyika kwa njia ambayo hairidhishi kabisa. Miongoni mwa miradi katika wadi hiyo ambayo utekelezwaji wake haubainiki, licha ya fedha kuwa zimetumika, ni zifuatazo:- (a) miradi ya ujenzi wa barabara; (b) miradi ya maji; (c) usaidizi wa watoto wanohitaji msaada wa elimu na mafunzo ya kiufundi; (d) mafunzo ya udereva kwa vijana 50; na, (e) kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Sidende. Kwa hivyo, wakaaji hawa wanaomba Bunge la Seneti lichunguze kwa kina utekelezwaji wa miradi iliyokusudiwa kutekelezwa katika Wadi ya Bukhayo ya Kati kupitia Hazina ya Maendeleo ya Wadi na Serikali ya Kaunti ya Busia katika Mwaka wa Kifedha 2014/2015, na litoe mapendekezo sahihi ya kulishughulikia na kutatua swala hilo, ili wakaaji wa wadi hiyo wapate haki. Maseneta Waheshimiwa, kwa mjibu wa Kipengele Nambari 226 cha Kanuni za Bunge la Seneti, nitaruhusu maoni, mitazamo au ufafanuzi kuhusiana na dua hii kwa muda usiozidi dakika 30. PROPOSED FORMULA FOR DIVISION AND ALLOCATION OF REVENUE TOWARDS REALISATION OF THE SDGS This is a petition to the Senate by Mr. David O. Gesicho concerning a proposed formula for division and allocation of revenue towards realisation of Sustainable Development Goals (SDGs). Hon. Senators, pursuant to Standing Orders Nos.220(1)(a) and 225(2)(b), I hereby report to the Senate that the petition has been submitted, through the Clerk, by Mr. David O. Gesicho, a resident of Kakamega County, concerning a proposed formula for division The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}