GET /api/v0.1/hansard/entries/622222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 622222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/622222/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Khaniri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 171,
        "legal_name": "George Munyasa Khaniri",
        "slug": "george-khaniri"
    },
    "content": "Mr. Speaker, Sir, I am guided. Ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nitachangia kwa rufaa ambayo imeletwa katika Bunge hili na wakaazi wa Wadi ya Bukhayo ya Kati. Kwanza kabisa, niruhusu niwashukuru wazalendo hao ambao wamewasilisha ombi hili kwa kuwa macho na kutaka kujua ni maendeleo gani ambayo wanapata katika sehemu yao. Ugatuzi ulikuja kunufaisha wananchi mashinani; pesa zitoke hapa Nairobi ili ziwafaidi wananchi kwa maendeleo mbalimbali ambayo wanahitaji katika sehemu zao. Kwa hiyo ni muhimu sana viongozi walio mashinani, Members of County Assembly(MCAs) pamoja na gavana na ofisi yake, kuhakikisha ya kwamba kabla ya kufanya mradi katika sehemu yoyote katika kaunti yao, wazungumze na wakaazi ili watoe maoni yao kuhusu miradi ambayo wanapendekeza kutekeleza katika sehemu zao. Hatutaki waanzishe miradi bila kuhusisha wananchi ambao wanatarajiwa kufaidika kutokana na miradi hiyo. Hata katika kaunti yangu, nimeona miradi mingi ni ya kufaidisha watu binafsi wala sio wananchi. Kwa hivyo, itakuwa muhimu sana wananchi wahusishwe katika mipango ya miradi ya maendeleo. Mwisho kabisa, ninajua utaelekeza rufaa hii kwa Kamati na Sheria za Bunge zinatupatia muda wa siku 60 kushughulikia rufaa. Vile umesema, kuna maombi mengi ambayo yameletwa hapa, muda huo umepitwa na siku nyingi sana hata miezi mitatu au minne na bado Kamati hazijaleta ripoti yake. Kwa hivyo, tunaomba ofisi yako ihakikishe ya kwamba rufaa zinazowasilishwa kwa kamati, iwe ni muda ule uliowekwa katika Kanuni zetu za Senate – muda wa siku 60 wala isipite. Ninaunga mkono rufaa hiyo."
}