GET /api/v0.1/hansard/entries/622227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 622227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/622227/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "February 18, 2016 SENATE DEBATES 17 Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ombi langu ni kwamba rufaa hii itakapowasilishwa kwa kamati inayohusika, tungetaka Kamati hiyo iaangalie rufaa hiyo kwa haraka. Sio lazima ifikishe zile siku 60. Ikiweza kufanyika kwa siku 10, tungependa ripoti hiyo iwasilishwe hapa mapema ili tuijadili. Vile vile, ninaomba tuangalie maombi ambayo yalikuwa yamepelekwa kortini kuhusu fedha za wodi ambazo zinasimamiwa na waakilishi wa Wadi, ili tujue kama ni haki wao kufanya hiyo kazi. La pili ni kwa lile dua ambalo limeletwa na Bw. Tedy Mwambire ambaye ni Naibu wa Spika kule Kaunti ya Kilifi. Fedha zinachelewa sana kutoka kwa serikali kuu na mwongozo wa Bajeti ya mwaka huu, utapata kati ya Kshs2,087,000 ni 34 asilimia ama karibu Kshs100,000,000 ambazo zimetolewa kufikia Disemba mwaka uliopita. Kwa hivyo, huenda tunauliza magavana maswali ilhali sio makosa yao. Lazima swala hili liletwe katika hili Bunge la Seneti. Hata hivyo, tukumbuke pia jana kuna Seneta ambaye aliuliza mwongozo kwa hili jambo na tutapokea taarifa hiyo kwa muda wa wiki mbili zijazo. Taarifa hiyo itatusaidia sana kwa kutoa mwongozo kuhusu jambo hilo."
}