GET /api/v0.1/hansard/entries/622846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 622846,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/622846/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii nami nichangie Mswada huu. Kwanza, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ni mzuri. Mswada huu utampatia nguvu Msimamizi wa Bajeti katika kufanya kazi yake. Kipengele cha 226 cha Katiba yetu ya Kenya kimeonyesha wazi wazi Msimamizi wa Bajeti na jinsi majukumu yake yanavyostahili kufanywa. Katika Mswada huu, tumeona kuwa kazi kubwa ya Msimamizi wa Bajeti ni kuhakikisha kuwa pesa zote ambazo zinakusanywa kutoka kwa umma zimepangwa kwa njia sawa na kutumiwa kwa hali ambayo zimepangiwa. Katika Bunge hili, ni bora kuhakikisha kuwa afisi ya Msimamizi wa Bajeti imepewa nguvu. Ili afisi hii ipate nguvu, ni lazima Bunge hili lipitishe pesa za kutosha kufanya kazi yao. Tunajua kuwa kazi ile ni ngumu kwa sababu inafaa kuhakikisha kuwa pesa zote ambazo zinakusanywa kutoka mifuko ya wananchi wa Kenya zinatumiwa katika njia ya sawa. Hii sio kazi rahisi kwa sababu wakusanyaji wa pesa hizo huzikusanya lakini mara nyingi hesabu zinazotolewa hazilingani kwa sababu huishia katika mifuko ya watu. Ni muhimu kwa Bunge hili kuipatia nguvu afisi hii ya Msimamizi wa Bajeti ili iweze kufanya kazi yake sawasawa. Kwa hayo machache, ninataka kuwa miongoni mwa Wabunge ambao wameunga mkono Mswada huu kuona kuwa Mswada huu utatupeleka mbele. Mara nyingi, sisi wanasiasa tunapeana nguvu kwa afisi fulani kufanya kazi kisha baadaye tunarudi na kuzipeleka afisi hizo kwa njia ambayo sio ya sawa. Kwa hivyo, afisi hii ya Msimamizi wa Bajeti inatakikana ifanye kazi yake kwa kujitegemea sawasawa bila kuingiliwa na mtu yeyote. Asante sana kwa kunipatia fursa hii kuchangia. Shukran."
}