GET /api/v0.1/hansard/entries/62298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 62298,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/62298/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Spika, nia kubwa ya Halmashauri ya Ziwa Viktoria ni hukakikisha kuwa Wakenya wengi wamepata maji kwa matumizi ya kila siku. Ni mipango gani halmashauri hii imeweka kuhakikisha kwamba watu ambao ni wakaazi wa chemichemi za maji wamepata maji ili wazihifadhi chemichemi hizo? Ninasema hivyo kwa sababu kuna bomba linaloelekea Mkoa wa Magharibi, lakini chemichemi iko katika Eneo Bunge langu. Bomba hili linapitia Taarafa ya Kaplamai, lakini kwa sasa wengi wa wakaazi hawaoni manufaa ya maji hayo. Sasa imekuwa ni kama wale wakaazi kazi yao ni kushika ng’ombe pembe na wengine wanakamua wakiwa upande wa chini. Wizara ina mipango ipi kuhakikisha kwamba wakaazi wa tarafa hii, ambao wanahifadhi chemichemi hizo, wanapata maji ya kutosha?"
}