GET /api/v0.1/hansard/entries/624477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 624477,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624477/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Spika. Ninaona Mwenyekiti ana wasiwasi. Nilikuwa nikitafuta tafsiri ya Kiswahili ya Ripoti hii lakini ninashukuru, imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Nitachukua nafasi hii kuwatafsiria wale ambao labda lugha ya kimombo inawaletea shida. Tumeisoma na kuielewa Ripoti hii. Ninaomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Wanachama wa Kamati husika. Hii inaonyesha wazi kwamba ukichukua fimbo na kuwachapa watu fulani, wanaamka. Tulipomwambia Mwenyekiti hapa kwamba wanazembea katika kazi yao, walifanya bidii na kuhakikisha kwamba ripoti hizi zimeletwa Bungeni na hivi sasa zinashughulikiwa."
}