GET /api/v0.1/hansard/entries/624478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 624478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624478/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ninaomba ripoti kama hizi zinapofika Bungeni na kujadiliwa, Kamati Tekelezi – ambayo inahitajika kutekeleza maamuzi ya Bunge – iyatekeleze maamuzi hayo. Sioni maamuzi ya Bunge yakitekelezwa. Ninasema hivi kwa sababu niko na ushahidi kuhusu ripoti nyingi ambazo zimepitishwa na Bunge hili lakini mpaka sasa hakuna pendekezo lolote ambalo limetekelezwa. Kamati ambayo inahusika na masuala ya sukari imetueleza na kufafanua jinsi hali ilivyo duni katika sekta ya sukari humu nchini. Tunasubiri tuone iwapo Kamati Tekelezi itafuata maagizo ya Bunge, ambayo yameandaliwa na kila mtu ameyasoma na kuyatilia maanani ili tuyafuatilie."
}